Pages

Tuesday, February 2, 2016

Zijue faida za Tangawizi kwa afya ya mwili wako

Tangawizi    ina  faida  nyingi  sana  kwa  mwili  wa  mwanadamu. Baadhi  ya  faida hizo  ni  kama  ifuatavyo :
1. Kutibu kutokusagika kwa chakula tumboni,.
2. Kutibu  tatizo  la gesi tumboni
3. Kuondoa  tatizo  la  msokoto wa tumbo (bila kuharisha)
4. Husaidia  kuzuia  kutapika.
5. Mshtuko/Mkazo wa ghafula (wa msuli),
6. Maumivu ya tumbo na Kibofu cha mkojo ikiambatana na Homa, Mafua, Kukohoa na Pumu.
JAM  YA  TANGAWIZI.
Unaweza  kutumia  Jam  ya  Tangawizi  kujitibu  magonjwa  mbalimbali  kama  ilivyo  onyeshwa   hapo  juu.
      
JINSI  YA  KUTENGENEZA  JAM  YA  TANGAWIZI. 
Kamua TANGAWIZI mbichi kisha changanya maji yake (Juice) na Sukari. Chemsha mpaka mchanganyiko huo uwe mzito. Ongeza Zafarani iliyosagwa,Iliki iliyosagwa, Kungumanga zilizosagwa na karafuu iliosagwa. Iweke dawa hii vizuri na tumia inapo hitajika.
MUONGOZO  WA  KUJITIBU  MAGONJWA  MBALIMBALI  KWA  KUTUMIA  TANGAWIZI.
Unaweza  kujitibu  magonjwa  mbalimbali  kwa  kutumia  zao  la  Tangawizi  kwa  kufuata  maelekezo   yafuatayo :
KUJITIBU   TATIZO  LA  KUVIMBIWA  NA  KUKOSA  HAMU  YA  KULA. 
Changanya Juice ya TANGAWIZI, Juice ya Limau na Chumvi Mawe kwa vipimo vilivyo sawa. Hakikisha umechanganya vizuri. Kunywa dawa hii kabla ya Chakula.
Vingineyo changanya vipimo vilivyo sawa sawa vya Juice ya TANGAWIZI na Sukari Mawe. Koroga vizuri, kunywa kabla ya kula chakula. Dawa hii husafisha Ulimi na Koo na hukuongeza hamu ya kula na kukufanya mchangamfu.
KUJITIBU   TATIZO  LA  MAUMIVU  YA  KUKOO  NA  KUKAUKA  SAUTI
Tafuna vipande vidogo vya Tangawizi.
 KUJITIBU   TATIZO  LA  KUHARISHA.
Chua sehemu zinazozunguka kitovu kwa Juice ya Tangawizi.
KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA
Kunywa mchanganyiko wa Juice ya Tangawizi na Juice ya Kitunguu.


MAUMIVU YA KICHWA CHA WASIWASI
Changanya Juice ya Tangawizi na Maziwa, kisha kausha. Nusa unga huo kama Tumbaku.


MAUMIVU MAKALI YA TUMBO
Changanya kijiko kimoja cha au viwili vya Tangawizi iliyosagwa na kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya Kastoroli. Kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku.
BARIDI YABISI SUGU
Changanya kijiko kimoja cha Tangawizi ya unga na vijiko 24 vya maji kunywa mchanganyiko huu ukiwa vuguvugu. Ulale na ujifunike mpaka utoe jasho.


KUUMWA JINO NA MAUMIVU YA KICHWA

Chukua Tangawizi ya Unga koroga na maji kidogo iwe nzito kama tope. Jipake na uchue kwenye paji lako la uso kabla ya kulala. Kwa Jino jipake na uchuwe kwenye Shavu.

0 comments:

Post a Comment