Pages

Tuesday, February 2, 2016

Umuhimu wa Asali Mbichi

Asali mbichi imekuwa ikitumika kama dawa na mataifa kwa matatizo mbalimbali kuanzia kwenye kikohozi hadi vidodnda vya moto.

Mdau asali unaitumia kwa matatizo gani? Mie natumia asali mbichi kuchanganyia tangawizi na limao ajili ya kikohozi. Pia asali mbichi peke yake huwa nawapaka watoto kwenye michubuko/viji-jeraha wanayopata kwenye michezo.
Ukweni kwangu sana sana wanachanganya asali na unga wa mdalasini (Cinnamon), viungo tutumiavyo kwenye pilau ajili ya kupunguza Blood Cholesterol Levels, kupunguza maumivu ya Arthrities, kuumwa jino, kuvumbiwa na pia ajili ya kikohozi na flu kwa ujumla. Pia asali tupu yatumika kwenye mwili (ngozi) kuondoa vijipele na ngozi inakuwa laini nyororo hivyo kuifanya asali kuwa mkorogo wa asili kwa wale wapenda mikorogo.


Je wewe unaitumia vipi? Naomba tubadirishane mawazo na wengine tufaidike zaidi na matumizi ya asali.

0 comments:

Post a Comment